MSWAHILI NI NANI
Dhana ya "Mswahili"
Dhana ya "mswahili ni nani?" ni dhana pana na
imejadiliwa na wanataaluma mbalimbali.
Uwepo wa mjadala huu umetokana dhana ya
Mswahili kuwa tata kwa "Waso- Waswahili" lakini pia na
"Waswahili"
wenyewe (Massamba:2002)
Hivyo ikaonekana haja ya kumfasili
Mswahili ili kutataua mgogoro huo
na kumpa uhalali wa kuwepo na kutumia lugha yake ya Kiswahili.
Kuna wanazuoni mbalimbali waliojadili dhana ya Mswahili.
Wataalamu wafuatao walijaribu kutoa
maana ya Mswahili
Kwa mujibu wa Stigand
(1913), anaeleza kuwa "Mswahili" ametokana na uzao wa mmojawapo wa
Waarabu, au Waarabu na Waajemi walioishi
katika upwa wa Afrika Mashariki.
Vilevile Steer (1870), anaeleza kuwa Mswahili ni mtu mwenye
mchanganyiko wa Kinegro na Kiarabu.
Nae Prins (1967)
ambaye anafafanua maelezo ya watu
wengine juu ya dhana ya Mswahili na mawazo hayo yanamnasibisha Mswahili na Mwarabu.
Na Ponera (2010),
Mswahili ni mtu mwenye kiwango kikubwa cha umilisi wa lugha ya Kiswahili. Vilevile
, ni mtu ambaye amefungamana sana na mila na desturi za jamii ya watu watumiayo
lugha ya Kiswahili kiasi hata cha kumuathiri kifikira, kimtazamo na kiitikadi.
DAFINA YA KISWAHILI
INAELEZA DHANA
YA MSWAHILI:
Kutokana na mtazamo hiyo na dhana na maendeleo ya lugha ya kiswahili, inaonekana wazi kuwa ni vigumu kumpata mswahili ambaye ni mmiliki wa lugha hii ya kiswahili. Inaonesha dhahili kuwa mswahili anaweza kutazamwa kwa namna tofauti kama zifuatazo;-
i). Mswahili anaweza kuwa ni mtu mahuruti yaani ni mtu chotara ambaye ni lazima awe ametokana mwingiliano wa pande mbili ambao ni wabantu na watu wanaonasibishwa na Waarabu
ii). Mswahili anaweza kuwa ni mtu wa mjini aliyeacha dini, utamaduni, mila na desturi zake za asili na kukimbilia dini, utamaduni, mila na desturi kutoka mataifa mengine kutoka uarabuni na nchi za kimagharibi
iii). Mswahili anaweza kuwa ni mtu ambaye anazungumza vizuri lugha ya kiswahili kwa kufuata taratibu zote za kiisimu na utamaduni wa lugha ya kiswahili
iv). Mswahili anaweza kuwa ni mkazi wa ya Afrika Mashariki hususani paeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki.
v). Mswahili anaweza kuwa ni mtu anayeishi katika maeneo ya kawaida ya mjini (uswahilini)
vi). Mswahili anaweza kuwa ni mtu ambaye ni mwafrika asili, anayepatikana katika nchi za Kenya na Tanzania
v). Mswahili ni mtu mwenye maumbile na ya kiafrika, ikimaanisha kuwa ni mtu wa miraba minne.

MAREJEO YA ZIADA
Massamba, D.P.B (1995) 'Lahaja
na Mitindo katika Kiswahili Sanifu' katika
Kiango, J. (mh),Dhima ya
Kamusi katika Kusanifisha Lugha. uk. 1 - 17.
Steere, E. (1930) A handbook of the Swahili
Language. East African Language
Committee
Stigand,
C.H. (1915) Dialects in Swahili. Cambridge University Press
Ponera, A.S. and
Luhwango, N. (2015), Riwaya ya
Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Labda,ukizungumza mswahili.
ReplyDeleteIkisema ni mtu kutokea mkoa na pamoja na Mila na destuli na kwa ujumla wao walivyo na katika maishilio.
Tafadhali Mwalimu Mkindi,ingalifahamika Kwanza kuhusu hili.
Asanteni sana kwa kunifungua akili. Nimekuwa nikisikia watu wanamchukilia mjanga mjanja kuitwa mswahili hii nayo inakoje?
ReplyDelete