RIWAYA YA KISWAHILI
NUKUU ZA SOMO:
MAANA YA RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA:
Riwaya
imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwao nikama vile,
Encyclopedia Americana
(EA), Jz. 20 (1982:510f) wakinukuliwa naMulokozi
(1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni inayotosha kuwa kitabu.
Udhaifu;
Maelezo haya yanaibua utata kwani hayafafanui kitabu kinapaswa kuwa na urefu
kiasi gani. Matharani kwa mujibu wa UNESCO katika Mulokozi (1996) kitabu ni
chapisho lolote lenye kurasa 48 au zaidi. Ama urefu wa kitabu hautegemei idadi
ya kurasa tu pia unategemea ukubwa wa kurasa (upana na kina) ukubwa wa
maandishi na mpangilio wake.
Encyclopedia Britanica
EB, Jz.8, (1985:810) wakinukuliwa naMulokozi
(1996) wanaeleza kuwa, riwaya ni masimulizi marefu yakinathari yaliyochangamana
kiasi, yenye kuzungumzia tajriba yamaisha ya binadamu kwa ubunifu.
Udhaifu:
Udhaifu wa hoja hii ni kwambawamejikita katika kigezo cha urefu, lakini hatujui
urefu huo wapaswa kuwa kiasi gani.
Wamitila (2002) Senkoro(2011) na hawakubaliani
na kigezo cha kufasili riwaya kwa kutumia
kigezo
cha urefu. Mfano Senkoro anaeleza kuwa ,“Ikiwa tutakichukua kipimo cha jumla
ya maneno(75,000)kuwa kielelezo cha riwaya basi itaonekana kuwatunariwaya
chache mno katika fasihi kwa hali hiinadhani sifa ya mchangamano ni nzuri
zaidikuelezeamaana ya riwaya” (uk. 56)Naye Wamitila anendelea kuelezea
kuhusiana na suala urefu kuwa,“Kigezo hiki cha urefu hakifaitunapoziangalia
kaziza fasihi ya Kiswahili...Mfano kazi mbili zaE. Kezilahabi,“Nagona
naMizingile” hazina idadi kubwa yamaneno lakinini riwaya”.
Wamitila (2002) na Senkoro (2011)
wanasema riwaya nikisa mchangamano ambacho huweza kuchambuliwa kupimwa
kwamapana na marefu kifani na kimaudhui.
>>
Riwaya ni kisa aumkusanyiko wa visa, nyenye urefu unaoviruhusu vitambe
nakutambaa mahali pengi na kuambaa vizingiti vingi vya maisha kamaapendavyo
mwandishi wake.
>>
Riwaya basi ni hadithi ndefu ya kubuni,yenye visa vingi, wahusika zaidi ya
mmoja, na yenye mazungumzona maelezo yanayozingatia kwa undani na upana, maisha
ya jamii.Riwaya hutoa picha ya jumla ya maisha ya mtu toka nyumbani hadikatika
kiwango cha taifa na dunia nzima.
Madumula
(2009), Riwaya ni masimulizi marefu ya kubuni yaliyo katika mtindo wa kubuni yakisawili
mtindo maalumu na madhumuni maalumu. Mhusika katika Riwaya anakuwa ni kipaza
sauti cha mwandishi.
KWA UJUMLA;riwaya ni
masimulizi ya kubuni ya kinathari yenye msuko au mpangilio fulani wa matukio au
ploti inayofungamana na wakati au kusawili wakati na yenye visa vingi
vivavyotendeka katika wakati fulani na yenye mawanda mapana yenye mchangamano
wa dhamira, visa na wahusika.
MAANA YA RIWAYA
KISWAHILI:
Riwaya ya
Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na utamaduni wa jamii ya waswahili katika
lugha ya kiswahili ambao hupatikanakatika nchi ya Afrika mashariki. Pia ni ile
riwaya ambayo inawahusu waswahili wenyewe.
VIPENGERE VYA MSINGI
KATIKA RIWAYA;
Inaonyesha
kuwa ili kujua maana ya riwaya ni vyemakuzingatia mambo kadhaa ambayo ndiyo ya msingi, na mambohayo
ni;
1) Lazima riwaya iwe na lugha ya kinathari,
2) Isawiri maisha ya jamii,
3) Iwe na masimulizi ya
kubuni na visa virefu,
4) Wahusika zaidi ya
mmoja,
5) Iwe na mpangilio na
msuko wa matukio,
6) Lazima na maneno kuanzia elfu thelathini na
tano na kuendelea, na
7) Riwaya ni lazima
ifungamane na wakati yaani visa na matukio ni lazima viendane na matukio.
HISTORIA FUPI YA
RIWAYA:
Riwaya
ilizuka kutokana na maendeleo ya mageuzi ya kiutamaduni. Suala la ukoloni na
uvumbuzi pia liliumba hali ambazo zilihitaji kuelezwa kwa mawanda zaidi ya yale
ya ngano na hadithi fupi. Hapo hapo kuzuka kwa miji na viwanda pamoja na
maendeleo ya wasomaji yalifanya riwaya nyingi ziandikwe.
Uchangamano
wa maisha ya jamii kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wenyewe ulizusha haja ya
kuwa na utanzu wa fasihi ulio na uchangamano kifani na kimaudhui.
Kupanuka
kwa usomaji, hasa wakati wa mapinduzi ya viwanda huko Ulaya, kuliwafanya
waandishi waandike waandiko marefu kwani sasa walikuwapo wasomaji hasa wanawake
waliobaki majumbani wakati waume zao walipokwenda viwandani, wasomaji ambao
muda wao uliwaruhusu kusoma maandiko marefu marefu ijapokuwa hii lilikuwa jambo
la baadaye sana wakati wa kina Charles Dickens. Hii historia fupi ya chimbuko.
Senkoro (2011:55).
HISTORIYA KATIKA RIWAYA
YA KISWAHILI;
Tanzu
za asili zinaonyesha kuwa ndio zilichangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibua
riwaya za Kiswahili.Na yafuatayo ni mawazo ya wataalamu mbalimbali juu ya
chimbuko la riwaya ya Kiswahili.
Madumulla
(2009), ameeleza kuwa riwaya ilitokana na nathari bunifu simulizi kama vile
hadithi, hekaya, na ngano inayosimuliwa kwa mdomo. Anaendelea kusema kuwa
fasihi ilitokana na maandiko ya fani ya ushairi hususan ni tendi za Kiswahili
katika hati za kiarabu kwa sababu ndiyo maandishi yaliyotamba katika pwani ya
afrika mashariki. Wazungu na waarabu hawakubadilishana maarifa kwa urahisi na
hivyo pakapelekea kuwa na majilio ya taratibu za maandiko ya kinathari.
Mwanzoni riwaya zilitafsiriwa kwa Kiswahili toka katika lugha za ulaya na
kufanya riwaya za Kiswahili kutokea. Mfano wa riwaya hizo ni kama vile; Habari
za mlima iliyoandikwa na Sheikh Ali Bin Hemed (1980).
Senkoro
(2011) anaeleza kuwa riwaya zilizuka kutokana na maendeleo na mageuzi ya
kiutamaduni, uchangamano wa maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, na
kiutamaduni yaliyopelekea haja ya kimaudhui zaidi ya ngano na hadithi fupi.
Anaendelea kusema kuwa riwaya za kwanza zilitafsiriwa toka riwaya za kizungu
mpaka za Kiswahili, Anasema riwaya mojawapo ni ile ya James Mbotela ya Uhuru
wa Watumwa. Ndiyo riwaya ya kwanza kutafsiriwa kwa Kiswahili. Pia anaeleza
kuwa riwaya ni utanzu uliozuka kutokana na hali mahususi za kijamii. Riwaya
kama ile ya kiingereza ya Robinson
Crusoe
iliyoandikwa
naDaniel Defoe ni miongoni mwa riwaya za mwanzo.
Mulokozi
(1996) anaeleza kuwa chimbuko la riwaya ya Kiswahililipo katika
mambo makuu mawili ambayo; nifani za kijadi za fasihipamoja na mazingira
ya kijamii.Fani za kijadi za fasihi, Mulokozi anaeleza kuwa riwaya
haikuzukahivihivi tu bali ilitokana na fani za masimulizi yaani hadithi, na
ndipozikapatwa kuigwa na watunzi wa riwaya wa mwanzo. Fani hizozilizopata
kuchipuza riwaya za mwanzo ni kama vile; riwaya zakingano, tendi, hekaya,
visakale, historia, sira, masimulizi ya wasafiri,insha na tafsiri.
Ngano,
Mulokozi
anasema, kuwa ni hadithi fupi simulizi pia huwa nihadithi za kubuni na nyingi
hasa zinawahusu wanyama wakali, piazinahusu malaika, binadamu, mazimwi na
majini. Anasema kuwamara nyingi ngano huwa na msuko sahihi na wahusika wake ni
bapana wahusika hao ni mchanganyiko wa wanyama, mazimwi nabinadamu. Anatolea
mfano wa ngano zilizo chukua visa vya kinganokuwa ni kama vile riwaya ya Adili
na Nduguze ya Shaaban Robart(1952), Lila na Fila ya Kiimbila (1966),
Kusadikika ya Shaaban Robart(1951).
Hekaya,ni
hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio ya ajabuyaani yasiyokuwa ya
kawaida. Mara nyingi masaibu hayohufungamanishwa na mapenzi. Hekaya hizo zimepelekea riwaya zaKiswahili
kama vile; Hekaya ya Adili na Nduguze ya Sharban Robart(1952), hekaya
ya Ubeberu Utashindwa ya Kiimbila (1971), na Hekayaya A.J.Amiri, ya Nahodha
Fikirini, (1972).
Tendi
(utendi), ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa
wa kihistoria na wa kubuni, ambao waweza kuwa ni wa kijamii au kitaifa. Kwa
kawaida baadhi ya tendi zina sifa za kiriwaya ila tu badala ya kuwa na umbo la
kinathari zenyewe zina umbo la kishairi. Kuna tendi za aina mbili ambazo ni
tendi andishi na tendi simulizi. Riwaya pevu kama tendi husawiri mawanda mapana
ya kijamii na kihistoria. Huwa na wahusika wababe yaani mashujaa wenye
kuwakilisha pande zinazopingana. Mfano wa tendi ni kama vile; Utendi wa Vita
vyaWadachi Kutamalaki Mlima ya Hemedi Abdallah, (1895), Utendi war as
(Ghuli), utenzi wa Fumo liyongo wa Mohamed Kijumwa K.(1913).Tendi katika
riwaya za Kiswahili imetumia wahusika wawili tuambao ni wahusika wa kubuni na
wale wa kijadi wa kiafrika.
Visasili,
hizi
ni hadithi zinazohusu asili na hatima ya watu, vitu,viumbe, ulimwengu na
mataifa, na pia huangalia uhusiano wawanadamu na mizimwi pamoja na miungu.
Hadithi za kivisasilizinapoonyeswa huaminika kuwa yakweli tupu hasa kwa
kusimuliamatukio mengi ya kiulumwengu.Mfano wa visasili; Lila na Fila ya
Kiimbila (1966) ambayo imekopamotifu ya asili ya ziwa ikimba huko Bukoba.
Hadithi ya Mungu waKikuyu huko Kenya. Roza Mistika ya Kezilahabi
(1971), Nagona(1987) naMzingile (1991), Siku ya Watenzi Wote ya
Sharban Robart.
Visakale,
ni
hadithi ya kale kuhusu mashujaa wa taifa,kabila au dini. Mara nyingi visa kale
huchanganya historia na masimulizi ya kubuni, na hadithi hizi hupatikana karibu
katika kila kabila kila lugha.Baadhi ya visakale vya Kiswahili masimulizi
huhusu chimbuko la miji ya pwani, mijikenda, mwinyi mkuu huko Zanzibar.Visa
kama hivi ndivyo vinavyopelekea kuandikwa kwa riwaya za kiswahili. Mfano wake
ni riwaya ya Abdalla Bin Hemed bin Ali Ajjemy (1972) katika kitabu cha Habari
za Wakilindi, Kisima cha na Giningi ya M.S.Abdulla (1968) na ile
Hadithi ya Myombekela na Bibi Bugonoka na Ntulanalwo naBuhliwali (1980)
ya A. Kitereza.
Masimulizi
ya kihistoria, haya ni masimulizi ya matendo ya,
mwanadamu katika muktadha wa wakati, na ni fani muhimu sana katika jamii yeyote
ile. Masimulizi halisi ya kihistoria yaweza kuwa ni ya mdomo au hata maandishi
na yote huwa ni chemichemi nzuri ya riwaya. Mfano wa riwya hizo ni; Habari
za pate za Fumo Omari Nabhany (1913) ambayo yalikuwa ni maandishi ya
masimulizi na uchambuzi. Riwaya zingine zilizoathiriwa na matukio ya kihistoria
ni;Uhuru wa Watumwa ya J. Mbotela (1934), Kifo cha Ugenini ya O.
Msewa (1977), Kwa Heri Iselamagazi ya B. Mapalala (1992) na Miradi
Bubu ya Wazalendo ya G. Ruhumbika (1992).
Sira,
ni
masimulizi ya kweli kuhusu maisha ya mtu au watu. Sira iliathirikuchipuka kwa
riwaya hasa kwa kuonyesha masilimulizi ya maishaya mtu toka utotoni mpaka
uzeeni. Masimuliza ya riwaya hiziyalikuwa katika masimulizi na hata katika
maandishi pia kwa maanakabla ya ukoloni yalikuwepo maandishi yaliyohusu maisha
ya mitumena masahaba.Mifano ya hadithi hizi ni; Kurwa na Doto ya M.
S.Farsy(1960),Rosa Mistika ya Kezilahabi (1971),Kichwa Maji ya
Kezilahabi(1974) pamoja na Dunia Uwanja wa Fujo (1975),Mzimu wa Baba
waKale ya Nkwera (1967),na riwaya ya Maisha Yangu baada ya MiakaHamsini ya
Sharban Robart (1951).
SIFA ZA RIWAYA;
Kwa
mujibu wa Wamitila (2002) sifa hizo ni
kama zifuatazo;
i)
Uwazi na uangavu,
ii)
kazi husika ya fasihi isiwasumbue nakuwatatiza wasomaji kuzielewa,
iii)
muwala na muumano,
iv)
kazi yariwaya lazima iwe na
mshikamano au mtiririko mzuri wa visa aumatukio kuijenga kazi ya kifasihi,
v)
uchangamano wa visa yaanikutokea kisa zaidi kimoja,
vi)
Wingiwa maana kuhusiana na sifa yauchangamano na ukamilifu ni kule
kuwako kwa elemeti zotemuhumiu na za kimsingi katika kazi ya fasihi.
SIFA NYINGINE NI:
vii)
Riwaya haifungwi na sheria wala
kanuni.
viii)
Riwaya ina matumizi ya lugha ya kinathali. Ni lugha ya mjazo wa
maneno na mtiririko wa mawazo.
ix)
Riwaya ina urefu na upana wa kutosha,,,,,, urefu na upana wa kimaudhui unapelekea kubeba
vijitanzu vingine vidogovidogo ndani ya Riwaya.
x)
Riwaya zao la kibepari: Riwaya ilizuka katika mfumo wa kibepari huko
Ulaya , Riwaya ina sifa ya ubinafsi, ina uhitaji mkubwa wa viwanda nah ii
ilianza ktk kipindi cha mapinduzi ya viwanda hivyo inahitji uchumi madhubuti
kama vile uandishi na uchapaji.
xi)
Riwaya iko karibu na uhalisia, inahusisha masimulizi ambayo
yalikuwepo,,,,, yapo,,,,,au yanatazamiwa yatokee na whusika hujengwa katika
mazingira hayo.
xii)
Riwa inahitaji ujuzi wa kusoma na kuandika.
xiii)
Riwaya inahitaji maisha tulivu,,,,, maisha anbayo yatamfanya mtunzi awe
katika hali ya kutunga Riwaya.
AINA ZA RIWAYA:
RIWAYA ZINAGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAKUU
MAWILIAMBAYO NI
(A) RIWAYA DHATI; Hizi ni Riwaya ambazo zina mambo dhati,
wasaha na manbo ambayo ni adili kwa binadamu. Hutumia lugha fasaha, nyofu na
hakuna matusi. Mfano ‘Kosa la Bwana
Mussa’, ‘Mzimu wa Watu wa Kale’, ‘Utengano’ na ‘Almasi za Bandia’.
(B)
RIWAYA
PENDWA;Hizi
huzungumzia maswala ya upelelezi, mapenzi na mambo mengine ambayo ni pendwa.
Riwaya pendwa huchomaza zaidi vipengere vya fani kuliko maudhui. Mara nyingi
hutumia methali, misemo na mbinu nyingine ambazo humfanya msomaji asitafakari
zaidi maudhui. Mfano: Pendo la Kifo, Njama, Kikosi cha Kisasi, Nyuma ya Pazia
na Mfadhili.
AINA ZA RIWAYA KWA KUZINGATIA VIGEZO
I)
KIGEZO CHA FANI:
Riwaya
sahili; ni dhana inayotumiwa kuelezea aina za riwaya
ambayo ina muundo rahisi na inaweza kueleweka kwa urahisi. Kwa mfano; riwaya ya
“Kaburi Bila Msalaba” ya P . Kureithi.
Riwaya
changamano; Ni riwaya ambayo ina muundo mgumu na inayohitaji
umakini kuielewa. Kwa kawaida msuko wa riwaya hii huwatata. Inawezekana
pakawepo na matumizi mapana ya mbinu rejeshi,upana mkubwa wa wahusika na
mandhari, matumizi mengi ya lughaya kitamathali, mfano; “Mzingile” ya E.
kezilahabi, “Zirail na Zirani” yaW.E Mkufya.
Riwaya
ya majaribio, Ni riwaya inayojadili mkondo wa nafasi
na riwaya kweli. Riwaya ya mjadara nafsi hutungwa bila kuzingatia kanuni za
kawaida za uandishi wa riwaya, watunzi wa riwaya hii hudai kuwa kumbo la
kawaida ya riwaya hii haitoshelezi mahitaji ya karne hii huwakilisha ukweli wa
maisha.Riwaya hizi hutumia nafsi ya pili na wakati mwingine hutumia nafsi mimi
kiasi kwa mwandishi ndiye mhusika. nafsi ya pili humfanya msomaji kuonekana
kuwa ndiye katenda jambo. Mfano, “Mtunzi wa Hukumu” ya Kasri na “Bina-Adamu” na
Musaleo” za Wamitila vilevile Nagona na Mzingire zake E, Kezilahabi.
II)
USIMULIZI:
Riwaya
barua ni riwaya ambayo huwa na muundo wa barua kuanzia
mwanzo hadi mwisho, au ni majibizano ya barua. mfano “Pamela” ya S.Richardson
na “ Barua Ndefu kama Hii.
Riwaya
ya kimonolojia ni riwaya ambayo sauti inayotawala ni
moja. Sauti hiyo ni ya mwandishi. Wahusika wanaopatikana katika riwaya hii
hudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na sauti ya mwandishi. Mfano “Walenesi” na
“Mafula” za Katama Mkangi.
III)
UPEO WA KIJIOGRAFIA:
Riwaya
ya kiambo; ni riwaya ambayo inatilia mkazo kwenye mandhari,
usemi au muundo wa kijamii na desturi za mahali maalumu. Mandhari na mahali
huathiri njia mbalimbali za kuhisi na kuwaza kwa wahusika wanaopatikana kazi ya
aina hii. Huelezea mambo ya tamaduni mfano, ‘Bwana Myombokera na Bi Bugonoka’,
watu wa Ukerewe na ‘Kisiwa Cha Giningi’.
Riwaya
ya kidastopia hii husawili jamii isiyokuwa ya kawaida
na isiyokuako kwa wakati maalumu bali inafikirika tu. Katika jamii hiyo sheria
za kawaida za kijamii zimebadilishwa kwa namna inayowafanya watu wengi waishie
kutaabika na kuteseka sana. Mfano wa riwaya hizi ni kama vile “ Kusadikika” ya Shabani Robert na
“Walenisi” ya Katama Mkangi.
Riwaya Kitaifa; hizi
hujikita katika upeo wa kijiografia ambapo haivuki mipaka ya nchi. Maudhui na
mawanda huwa ni yamambo yanayojiri katika taifa husika,
Riwaya za Kimataifa; Hi
ni Riwaya ambazo ni kinyume cha zile za kitaifa kwa hujadili mambo ya nchi
zaidi ya moja, mfano wan chi zinazoendelea na zilizoendelea.
IV)
MAUDHUI:
Riwaya
historia ni aina ya riwaya ambayo msingi wake kuhusu matukio
fulani katika jamii ya mwandishi, tukio hili huwa ni kubwa na la muhimu
kijamii, laweza kuwa la kikabila au la kitaifa mfano “Uhuru wa Watumwa” ya J.
Mbotela, “Miradi Bubu ya Wazalendo” ya Luhumbika na “Zawadi ya Ushindi” ya B.
Mtombwa.
Riwaya
ya kimaadili ni riwaya ambayo ina nia ya kufundisha
maadili fulani mfano “Kufikirika” ya
S Robert. Ni riwaya inayotoa maadili kwa jamii. Riwaya hizi huelezea mambo ya
dini, mafunzo na maonyo ya maisha. Hujengwa katika nguzo tatu ambazo
a) Mathema (kosa):
Kosa analolifanya mhusika mkuu linafanya jamii ipate shida. Kosa hilo humfanya
mhusika ajifunze na jamii ijifunze.
b) Pathema
(Funzo):Mafunzo anayoyapata mhusika juu ya kosa alilolifanya,
c) Cathersis (utakaso):
Utakaso unapatikana baada ya funzo na kubadilika.
Riwaya
ya kimapinduzi ni riwaya ambayo inajadili migogoro
namaisha ya binadamu kwa kutafakari kwa mantiki na kina kuhusumambo ambayo
urazini wake hauonekani kwa urahisi.Hudodosa mapambano, mikinzano na matabaka
katika jamii Mfano“Umleavyo” ya Haji na Kichwa Maji” ya E.Kezilahabi, vilevile
na Dunia mti mkavu na Kusadikika.
Riwaya ya kisosholojia au jamiini
riwaya ambayo inasawiri maisha ya kawaida ya jamii kwa kuchunguza matatizo
yake, yawe kifamilia kitabaka, kiuchumi, kisiasa au hata kiutamaduni mfano
“Titi la Mkwe” ya A. Banzi, “Kurwa na Doto” ya M.S. Farsi na “Rosa Mistika” ya
E. Kezilahabi.
Riwaya saikolojiani aina ya riwaya
inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia mawazo, imani, hofu, mashaka,
matumaini na athari ya mambo hayo kwake binafsi na labda kwa jamii mfano
“Kichwa Maji” ya E.Kezilahabi, “Kipimo cha Mianzi” ya Feud na “Kiu” ya M.S.
Mohammed.
Riwaya
ya kifalsafa, ni riwaya ambayo inashughulikia
masuala ya kifalsafa. Mada ya kifalsafa huchukua sehemu muhimu katika riwaya ya
aina hii kuliko wahusika, mandhari, msuko au mtukio.Mtunzi hutaka wasomaji
wafikirie kifalsafa mambo Kama vile kuwepo au kutokuwepo kwa MUNGU, Baadhi ya
viumbe, kufa na kuishi ni nini? Utu na mtu nini? Mfano, “Nagona na Mzingile” ya
E kezilahabi na “Umleavyo” ya Haji Gorra Haji.
Riwaya
ya mapenzi ni riwaya yenye kusawiri uhusiano wa
kimapenzi kati mvulana na msichana. Huchomoza zaidi fani kuliko maudhui, Mfano
“Kweli Unanipenda” “Mwisho wa Mapenzi” za Simbamwene.
Riwaya
ya kitawasifu, ni riwaya ambayo ina muundo unafanana
na muundo wa tawasifu kwa kuyachunguza maisha ya mtu fulani na kwa nafsi ya
kwanza. Mfano riwaya ya “Uhuru wa watumwa” J. Mbotela na “Maisha Yangu baada ya
Miaka Hamsini” ya S.Robert.
Riwaya
ya wasifu, ni riwaya ambayo mwandishi huandika kwa lengo la
kumhusu mtu fulani, mfano “Wasifu wa Siti Binti Saad” ya S. Robert.
KUNA MAKUNDI MENGINE YA RIWA AMBAYO
HAYAKUAINISHWA HAPO JUU NAYO NI:
Riwaya
ya ujasusi ni wa upelelezi wa kimataifa. Majasusi
ni wapelelezi wanaotumwa na; nchi, serikali au waajiri wao kwenda katika nchi
nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi, kiuchumi na kisayansi ili
taarifa hizo ziwanufaishe wale waliotumwa mfano “The thirty nine steps” ya E.
Msiba. “Mzimu wa Watu wa Kale”.
Riwaya
ya kisayansi ni riwaya inayotumia taaluma ya
sayansikama msingi wa matukio, masahibu na maudhui, mathalani riwaya
hiihubashiri namna sayansi itakavyo athiri maendeeo ya mwanadamukatika karne
zijazo. Mfano “Safari Kiini cha Dunia” ya Jules Vernes.
Riwaya
tendi ni riwaya yenye mawanda mapana kama tendiaghalabu
riwaya hii husawili matendo ya ushujaa na masuala mazitoya kijamii yenye
kuathiri historia ya taifa husika. Mfano “Vita naAmani” ya Leo Tolstoi na
“Chaka Mtemi wa Wazuru” ya Thomas M.
Riwaya
istiara ni riwaya mafumbo ambayo umbo lake la nje niishara
au kiwakilishi tu cha jambo jingine. Mfano “Kusadikika” yaS.Robert ambayo
inasawili utwala wa mabavu na “Shamba laWanyama” ya Kawegere
Riwaya
chuku ni riwaya ambayo hueleza vituko na masahibuyasiyo
kuwa ya kawaida, ni riwaya ambayo haizingatii uhalisia namara nyingi masahibu
yake huambatanana mapenzi.Mfano “Alfu lela
Riwaya
ya kingano, ni riwaya yenye umbo na mtindo wa nganomathalani
huweza kuwa na wahusika wanyama,visa vyenyekutendeka nje ya wakati wa
kihistoriA.Mfano “Lila na Fila” yaLongman na “Adili na Nduguze” ya S.Robert
Riwaya
kinzani ni riwaya inayotumiwa kuelezea ambayo
imekwendakinyume na matarajio au kaida za uandishi wa riwaya. Mfano, kuwana
muundo wa kimajaribio wahusika kukosa motisha, kuwako kwamatendo yasiyoweza
kuungwa kimantiki.
Riwaya
ya utetezi hii hutumiwa kuielezea riwaya ambayo
inahusumatatizo ya kijami, kiuchumi pamoja na dhuluma inayowapatawanyonge au
wasiokuwa na uwezo katika jamii fulani. Hivyo riwayahii hukusudia kurekebisha
hali iliyopo katika jamii. Mfano “Walenisi”na “Mafuta” ya Katama Mkangi na
“Kuli’ na “Vuta n’kuvute” za ShafiA.Shafi.
Riwaya
ya kipolifoni; ni riwaya ambayo inahusishwa na
urejeleaji ambapo kila wahusika wanapozungumza au kuongea sauti zaombalimbali
zinawakilisha mikabala mbalimbali kiitikadi. Mfano “Duniamti mkavu” ya S.A
Mohamed.
Riwaya
ya kisasa; ni riwaya inayohusu wanasiasa na maisha
yaowanasiasa. Hudhamiria kuyafichua mambo yanayotendeka kinyumena picha
inayoonekakana waziwazi. Mfano; “Nyota ya Huzuni” yaGeorge Liwenga na “Njozi
Iliyopotea” ya C.G. Mng’ong’o.
Riwaya
ya kitarihi ni riwaya ambayo inajihusisha na mawanda
makubwa ya kiwakati na kimandhari.Wahusika wengi walioteuliwakuakisi hali
mbalimbali za kijamii na kiuchumi za wakati maalumu.Mfano;Riwaya ya “Habari za
Wakilindi”
Riwaya
ya kiutopia hii ni riwaya ambayo inasawiri jamii
anayoionamwandishi kama jamii kielelezo na aghalabu huhusisha sifa zaKifantasia
au kinjozi. Mfano wa riwaya hii ni kama, “Siku ya WatenziWote” ya Shaaban
Robert.
Riwaya
ya kiurejelevu hii ni riwaya inayojirejelea. Aghalabu
katikausimulizi wake, riwaya ya aina hii huishia kutoa maoni kuhusuusimulizi
wake na njia za kubuni na kutunga riwaya.Tunawezakusema hii ni riwaya
inayofichua mbinu zake za kiutunzi. Mfano“Musaleo” ya K.W.Wamitila.
Riwaya
tatizo; ni riwaya ambayo inajishughulisha na tatizo
aumgogoro fulani katika jamii. Huweza pia kuelezea aina ya riwayaambayo
inachunguza tasnifu au swala fulani la kisaikolojia. Mfano;“Kuli” ya Shafi
A.shafi na “Mafuta” ya K. Mkangi.
Riwaya
kampasi; ni riwaya ambayo mandhari yake ni chuo kikuu. Hata
hivyo hii imepanuliwa nakuhusishwa na kazi za kuchekesha auzenye mwelemeo wa
kitashititi. Kazi za aina hii hukusudia kufichuaudhaifu uliopo katika tabia za
wanachuo.Mfano; “Small world” yaDavid Lorge.
NADHARIA
ZA UCHAMBUZI WA FASIHI
Wataalamu
mbalimbali wameainisha nadharia mbalimbali za uchambuzi wa kazi yoyote ya
fasihi. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja na;
(i)
Nadharia ya umuundo (structuralism)
Umuundo
ni nadharia inayojibainisha kwa kuangalia Ujumla wa uhusiano wa sehemu moja kwa
nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa mfano muungano wa maneno hufanya
sentensi na sentensi zikiungana zinaunda aya au onesho na onesho kuunda
tamthiliya. Ntarangwi (2004) anasema kuwa umuundo waweza kuelezwa kama mtizamo
wa kitathimini ambao huzingatia zaidi miundo inayojenga kazi binafsi.
Mwasisi anayetajwa sana katika nadharia hii ni
Ferdinard De saussure aliyependekeza mtizamo mpya kuhusu lugha. Kinyume na
wataalamu wengine walioshughulikia historia na sura maalum za lugha fulani,
Saussure alivutiwa na miundo inayohimili lugha zote, huku akijaribu kuonyesha
kwamba lugha zote za ulimwengu zaweza kutathiminiwa kwa kaida maalum za
umuundo. Alizua istilahi `parole' na `langue' kueleza maoni yake: `Parole' au
uzungumzi ni lughakatika matumizi na hiki ndicho walichokizingatia
wanaisimu wa awali,
Mkondo
huu wa mawazo ya umuundo kuhusu sayansi za jamii ulianzia ulaya na kuathiri
mtazamo wa elimu mbalimbali (duniani) kama vile: Falsafa, Anthropolojia,
Historia, Uhakiki wa kifasihi naSasiolojia. Kwa hivyo twaweza kuangalia jamii
katika muundo wake wa kijuu juu na kuielewa lakini tukitaka kupata maana
mwafaka lazima tuchunguze muundo wake wa ndani ambao hupatikana katika kila
jamii ya wanadamu. Kwa hiyo hata katika kuielewa fasihi lazima tuifahamu lugha
yake.
UMUUNDO NA FASIHI
Kama
vile muundo wa lugha ulivyo mfumo, muundo wa fasihi pia una vipengele
vinavyotegemeana na vinavyoelezwa katika muktadha wa vipengele vingine. Katika
kazi ya fasihi kuna kitengo cha kisanaa kama vile maudhui, ploti, wahusika,
muktadha na lugha. Hakuna kipengele cha fasihi kati ya hivi kitakachoelezwa
katika upekee wake. Lazima kielezwe kwa kuzingatia kuwepo kwa jukumu la
vipengele vingine. Kwa mfano katika kueleza au kuzungumzia ploti, wahusika
watashirikishwa na lugha yao kuzingatiwa. Kwa hiyo nadharia ya umuundo
husisitiza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha
kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi za sanaa zilivyofungamana.
Yaani Neno halihitaji urejelezi ili lipate maana, na Kazi yenyewe ilivyoundwa
ndivyo hutoa maana. Yaani maana inavyoumbwa ina dhima kubwa kuliko maana
yenyewe.
(ii)
Nadharia ya umarx (marxism)
Kwa
maana rahisi kabisa, tunapoongelea kuhusu nadharia ya UMarxtuna maana ya
kurejelea mikabala mbalimbali ambayo misingiyake mikuu ni mawazo yanayohusishwa
na Carl Marx na FriedrichEngels. Katika kitabu cha The
Germany Ideology, Marx na Engelswalisema kuwa kitu cha msingi katika
maisha ya binadamu ni kula nakunywa, kupata malazi na mavazi na mambo
mengine. Tendo lakwanza la kihistoria kwa hiyo ni kutafuta njia ya kuyakidhi
mahitajihaya ya msingi. Ili kufanikiwa katika lengo hilo, binadamu
hulazimikakujiunga pamoja au kuunda umoja ili kuimarisha umoja na wepesi wakuizalisha
mali ya kukidhi mahitaji hayo. Muungano huo huwa naugawaji wa majukumu au kazi
ambayo ndiyo msingi wa kuundwakwa matabaka katika jamii.
Umarx
katika Fasihi
>Usanii
ni uumbaji wa Ukweli katika maisha.
>
Ukweli unaooneshwa katika kazi za fasihi hiyo ni usahihi wa mambo katika jamii?
Kama niRiwaya, Tamthilia, Ushairi na kadhalika inawakilishaje ukweli?
>
Kazi za kisanaa zinatakiwa kuonesha mivutano iliyopo katika jamii hasa kati ya
wanyonyaji na manyonywaji.
(iii)
Nadharia ya urasimi
Kwa
mujibu wa Njogu na Wafula (2007) Urasimi ni wakati maalumuambapo misingi ya
kazi za sanaa huwekwa na kukubalika kuwavipimo bora kwa kazi nyingine. Hii ina
maana kwamba kila jamii inaurasimi wake. Urasimi katika Kiswahili ulikuwepo
kati ya karne ya 18na karne ya 18. Nao urasimi wa Kigiriki ulikuwepo baina ya
karne yanne (KK) na takriban karne ya nne (BK).
Sifa
za urasimi kwa ujumla
Pamoja
na kwamba imeshatajwa hapo mwanzo kuwa kila jamii ina urasimi wake, lakini bado
tunaweza kutoa sifa za jumla za urasimi mahali popote ulipo. Kwa mfano:
>Kazi
ya kirasimi huwasilishwa katika lugha inayoeleweka kwa urahisi. Hii ina maana
kuwa wazo linaelezwa moja kwa moja. Mitindo ya Kinjozi (mf.Nagona, Mzingile,
Bina-Adamu, Walenisi) haitumiwi.Uhalisia unasisitizwa.
·>Kazi
nyingi za kirasimi hazichoshi kusoma. Hii ni kwa sababu kazi hizi ni kazi bora.
Husomwa mara nyingi na watu wengi na kila unapoisoma wazo jipya hupatikana.
>Fani
na maudhui katika kazi za kirasimi ni mambo yaliyofinyangwa kwa kutumia mbinu
kamilifu na teule. Daima kuna ufungamano uliokamilika kati ya kinachoelezwa na
jinsi kinachoelezwa.
(IV) JE
ONTOLOJIA YA KIAFRIKA INAWEZA KUTUMIKA KAMA
NADHARIA
YA KUCHAMBULIA KAZI ZA FASIHI ZA KIAFRIKA?.
( fuatiliya
makala hii katika mtandao ili kupata nukuu zaidi )
JE
UNGEPENDA KUJUA MAANA AU FASILI YA FALSAFA
Wikipedia
kamusi elezo huru wanasema,falsafa ni neno linalotokana na neno la kigiriki
lenye maana ya upendo na hekima,wanaendelea kusema kuwa falsafa ni jaribio la
kuelewa na kueleza ulimwengu kwa kutumia akili inayafuata njia ya mantiki .
Falsafa huchunguza mambo kama vile kuweko,au kutokuweko,ukweli,ujuzi
,uzuri,mema, na mabaya,lugha na haki.
Kwa
mujibu wa Wamitila (2003 ) anasema, falsafa ni mawazo anayoyaamini mtu au
mwandishi kuwa yana ukweli unaotawala misingi ya maisha.
Hivyo,
Falsafa ni taaluma au mtazamo unaochunguza matumizi ya dhana,kupima hoja,mbinu
za ujengaji hoja,kufanya uhakiki au tathimini,kuthibitisha au kutoa ushahidi wa
hoja zinazozungumzwananadharia mbalimbali zinazohusu maisha.Mfano,kuua ni tendo
zuri au sio zuri?
BASI
IMANI NA MTAZAMO WAKO VIKUONGOZE KATIKA KUSOMA NA KUTAFAKARI NUKUU HIZI:
NAKUTAKIA
USOMAJI MWEMA WA KISWAHILI (RIWAYA KISWAHILI);
Nukuu hizi ni baadhi zimekusanywa
kutoka wataalamu mbalimbali, Vitabu na mitandao ya kijamii; na
MWLIMU ALLY ABDUL MKINDI
NA AISHA ALLY
ABDUL MKINDI
MALEJEO.
Madumulla,
S.J. (2009) Riwaya yaKiswahili: Nadharia Historia na Misingi yaUchambuzi.Dar
es
Salaam: MtureEducational Publishers Ltd.
Mulokozi,
M.M. (1996) Utangulizi wa Fasihiya Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.
Senkoro,
F.E.M.K. (2011) Fasihi. Dar esSalaam: KAUTTU.
Wamitila,
K.W. (2002) Uhakiki wa Fasihi:Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi:Phoenix
Publishers
Ltd.
Wamitila,
K.W. (2003) Kamusi ya Fasihi:Istilahi na Nadharia. Nairobi: FocusPublicatins
Ltd.
Madumulla, J.S.
(2009), Riwaya ya Kiswahili, Historian a Misingi ya Uchambuzi. Nairobi:
Sitima Printer
andstations L.td.
Mulokozi, M.M.
(1996), Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam. TUKI.
Mhando, P. na
Balisidya, (1976), Fasihi na Sanaa za Maonyesho. Dar es Salaam: Tanzania
Publishing
House.
Nkwera, F.V.
(1978), Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: Tanzani
Publishing
House.
TUKI,(2004),Kamusi
ya Kiswahili Sanifu.Nairobi.Kenya:Oxford University Press.
Senkoro,F.E.M.K.(2011),
Fasihi Andishi.Dar es Salaam.Kauttu L.t.d.
Wamitila,K.W.(2003),Kamusi
ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Nairobi:Focus Publication.
Mihanjo A,(2010)Falsafa
na ufunuo wa maarifa.Toriam.MorogoroTanzania.
Mohamed S.k
(1988)Fungate ya uhuru.Dar-es-salaam universityplace(DUP).
Muhando p (1982)
Nguzo mama. Dar-es-salaam universityplace(DUP).
Njogu na Chimera
R(1999)Ufundishaji wa fasihi,Nadharia naMbinu.Jomo Kenyatta.Nairobi
Tuki(2004)Kamusi
ya Kiswahili sanifu.Taasisi ya Uchunguzi waKiswahili.Dar-es-salaam.
Wamitila K.W
(1996) Utangulizi wa Kiswahili.Chuo kikuu cha
Dares-salaam.Dar-es-salaam.
No comments:
Post a Comment